Ringtone; Mimi Ni Tajiri Kuliko Diamond Platnumz, Naweza Kumhudumia Zari Kwa Kila Kitu

Alex Apoko anaefahamika kwa jina maarufu kama Ringtone ameendelea kurusha madongo kwa Diamond Platnumz. Muimbaji huyo wa Muziki wa Injili mwenye makazi yake Nchini Kenya amefunguka na kudai kuwa yeye ni tajiri kuliko Diamond hivyo anaweza kumhudumia mwanamama Zari.

Muimbaji huyo amewekea mkazo Kwenye suala lake la kutaka kukutana na mwanamke huyo aliyetangaza kuzika penzi lake na Diamond Kwenye usiku wa Valentine's Day.

Akipiga Stori na CitizenTV ya Kenya, Ringtone amesema alianza kuchezea mamilioni ya pesa kwa kuuza Muziki wake mashuleni.
   
"Ninamiliki biashara, Nafanya Kazi kwa bidii, Nina umri Mdogo, lakini mjasiriamali ambaye Tayari najiita tajiri" alisema Ringtone.

"Nina uhakika utajiri wangu ni mara mbili au zaidi ya utajiri wa Diamond, Naweza Kufanya kila kitu, naweza kutembelea choper, Nahisi naweza kumtunza ZaritheBossLady kitu ambacho Diamond ameshindwa.