Ushauri Wa Wema Sepetu Kwa Diamond Platnumz Na Zari Baada Ya Kupigana Chini

Queen wa Bongo Movie, Tz Sweetheart Wema Abraham Sepetu ametoa ushauri juu ya mahusiano ya aliyewahi kuwa Mpenzi wake ambaye ni Staa wa Muziki Diamond Platnumz na mzazi mwenzie Zarina Hasani a.k.a ZaritheBosslady baada ya Zari kutumia Usiku wa Wapendao kutangaza kuyavunja rasmi mahusiano ya kimapenzi Na Chibu

Akipiga story na Dizzim Online Wema amesema bora wamalize tofauti zao ili waendelee kuwalea watoto wao kwa pamoja kwasababu hakuna mahusiano yasiyokuwa na changamoto wala migogoro.

Kama kweli wameachana mimi naona wayamalize tu na maisha yaendelee ingawa mapenzi hayaingiliwi  warudiane ili walee watoto wao kwa pamoja” Amesisitiza mrembo huyo".

Pia Mrembo huyo amegusia suala la kupotelewa na Akaunti yake ya Instagram na kusema kuwa ni kweli imechukuliwa na amewaomba Mashabiki zake waendelee kuwa na moyo wa subira kwani bado anaendelea na jitihada za kuirudisha mikononi mwake.