Nywele Ndio Talk Of The Town, Baada Ya Alikiba Na Ommy Dimpoz Sasa Ni Vanessa Mdee

Wanamuziki Alikiba Na Ommy Dimpoz Wanaowakilisha RockStar4000 Waligeuka Gumzo Siku Ya Jumatatu Baada Ya Kuonyesha Picha Za Muonekano Mpya Wa Nywele Zao Ambapo
Alikiba Alionekana Kupaka Rangi Nyekundu Na Ommy Dimpoz Rangi Ya Brown.

Muonekano Wa Alikiba Na Ommy Dimpoz Umekuja Miezi Michache Baada Ya Ben Pol Ambaye Aliamua Kupaka Rangi Ya Kijani, Ben Pol Ambaye Anasemakana Kupitia Muonekano Wake Ameweza Kupiga Dili La Maana Alionyesha Kufurahishwa Na Muonekano Wa Wawili Hao Kwa Ku-comment Kwenye Moja Ya Picha Zao "Leo Nimefarijika Sana" Aliandika Ben.

Sasa Baada Ya WaRockStar Hao Kugeuka Maada Mitandaoni Hitmaker Wa "Cash Madame" Vee Money Naye Amedondoka Na Muonekano Huo Wa Kupaka Rangi Nyekundu Kichwani Huku Akiamini Ben Pol Amefarijika Zaidi.
"Naamini Ben Umefarijika Sana" Ameandika Vanessa Mdee Kwenye Picha Yake Yenye Muonekano Huo.

Wanamuziki Kubadili Rangi Za Nywele Zao Ni Sawa?
Weka Maoni Yako.