Kwenye Made From Miami, Camila Cabello Amekitaja Kilichomtoa Fifth Harmony, Maisha Kabla Na Baada Ya Umaarufu

Jana (February 27), Kwenye YouTube yake Camila Cabello aliiachia Documentary yake "Made In Miami".

KwaMujibu Wa makala hiyo Camila na Familia yake wamefunguka jinsi walivyonigia Marekani, Safari ya Kimuziki ya Camila kutokea X-Factor Mpaka Fifth Harmony, Na Mpaka Kilichopolekea kujiondoa Kwenye kundi hill lililompa Umaarufu.

"Nilipokuwa kundini nilijifunza vitu vingi ambavyo pia vilinikuza, Lakini baadae nilihisi kuna vitu vingi nahitaji kuzungumzia" alisema Camila. "Nadhani kwa Mimi kama mwanamuziki njia pekee ya kunifanya nijisikie vizuri ni Kufanya vitu ninavyovipenda, Lakini nilipokwenda kule sikuwa na uwezo Wa kuzielezea hisia zangu, Sikua Naweza Kuzielewa hisia Zangu, Hiyo ni sababu kwanini nilihisi nahitaji kubadili kitu"

Simon Cowell ambae ndiye alikuwa Boss Wa Camila ameelezea mshituko alioupata Baada ya kupokea taarifa Za Camila Kujitoa Kwenye Kundi hilo. "Nilikuwa Sijatarajia kupokea taarifa Hizo kwa Wakati zilionifikia, malengo yangu hayakuwa kumuacha Camila kwa kipindi kifupi tu Baada ya Mafanikio ya Fifth Harmony Lakini Baada ya kuganda Kwenye msimamo wake ilifika hatua nilitakiwa kuheshimu mammuzi yake."

 Kwenye Kauli nyingine Camila amesema "Kiukweli ilikuwa inaniumiza, Nilikutana na Vitu nilikuwa sitegemei, Mpaka nilipoamua kuondoka. Nilikuwa najiuliza Nini? Kwanini?, Lakini nikajipa moyo kwamba nataka Kufanya mambo makubwa Zaidi. " Sihitaji kufikiria yaliyopita, Nilichofanya niliona ni Sawa kwangu na waliohitaji vitu vizuri Kutoka kwangu" Alimaliza Camila.

2017/18 Imekuwa Miaka mizuri kwa Camila Cabello kwani Baada ya kuachana Na Kundi la Fifth Harmony ameendelea kung'ara Kwenye chati mbalimbali za muziki ikiwemo kuingiza Albamu yake Kwenye Billboard Top 200 na ngoma Yake Havanna aliyomshirikisha Young Thug kushikilia Nafasi ya Kwanza Kwenye Billboard Top 100.