Je, Kupotea Kwa Instagram Account Ya Wema Sepetu Ni Moja Ya Mipango Yake?

January 31 Kwenye Instagram Mastaa Wengi Wa Tanzania Walitupia Post Iliyobeba Maandishi June 30th 2018. Save The Date Na Caption Ilisomeka #TzSweetheart2018. Bila Kuchengesha Kila Mtu Aligundua Malkia Wema Sepetu Ana Tukio La Kushare Na Mashabiki Wake Ifikapo Tarehe Hiyo.

Hakikupita Kipindi Kirefu Account Ya Instagram Ya Wema Sepetu Ilitangazwa Kuibiwa Na Watu Wasioujulikana Kisha Kuanza Kupost Matangazo Ya Biashara Huku Ikiendelea Kuonekana Kwa Jina La @WemaSepetu Mpaka Hapo Ilipotoweka Kabisa Mwanzoni Kwa Wiki Hii.

Wema Sepetu Kupitia Application Yake Alishare Taarifa Za Akaunti Hiyo Kuwa Hacked Kwa Kudai Kuna Mtu Ambaye Amefanikiwa Kuiba Taarifa Za Msingi Ikiwemo Namba Ya Simu Na Email Ambazo Mrembo Huyo Alikuwa Akizitumia Kwenye Mtandao Huo.

Wakati Kila Mtu Akiongea Anachokifahamu Kuhusu Kupotea Kwa Account Hiyo Yenye Wafuasi (Followers) Zaidi Ya Milioni 3, Imani Yangu Inanishawishi Kusema Page Ya Wema Sepetu Haiwezi Kuwa Hacked Kirahisi Kutokana Na Mazingira Ya Mrembo Huyo Kwani Hakuna Nafasi Ya Mtu Wa Kawaida Kushika Simu Yake Mpaka Kukamilisha Mchezo Huo.

Kuwa Hacked Ni Mission Inayofanywa Na Mtu Wa Karibu Anayefahamu Kila Kitu Kuhusu Vitu Vyako Mtandaoni Nikiwa Ni Pamoja Na Email Password Na Namba Za Simu.

Tunajua Vile Timu Ya Wema Sepetu Inapambana Kwa AJili Yake Hivyo Hawawezi Kutekeleza Mpango Huo, Sasa Kama Sio Mtu Wa Karibu Nani Yuko Nyuma Ya Mchezo, Nani Alipokea Matangazo Yaliyokuwa Yakipostiwa Kabla?
Waliotangaziwa Walimlipa Nani?

Kutengeneza Followers Wengine Milioni 3 Ni Zoezi Ambalo Mrembo Huyo Atatakuwa Kuhangaika Nalo Si Chini Ya Miaka 2.

Kuna Muda Nathubutu Kusema Huenda Hii Ni Njia Ambayo Mrembo Huyo Ameitumia Kujiweka Kando Ya Mitandao Huo Kama Ambavyo Alikuwa Akifanya Kipindi Cha Nyuma Na Baadae Kurudi Kwa Mara Kadhaa.

Tukirudi Kwenye Post Inayotoa Alert Ya June30th Bado Tunakuwa Hatuelewi Kinachokuja Kutoka Kwenye Stoo Ya Wema Sepetu Lakini Tunatamani Kuona Tukio Hili Limeambatana Na Kurudishwa Kwa Account Hiyo Ikiwa Tu Kinachoendelea Ni Moja Ya Mipango Ya Wema Na Timu Yake.