Drake Amejibu Mapigo Kwa Kylie Jenner

Drake hajakubali Kubaki nyuma Kwenye Suala la kusukuma ndinga Kali, Baada ya Mrembo Kylie Jenner kuonekana Kwenye mitaa Ya Jiji La Los Angeles akiwa Kwenye gari Jipya Aina ya Ferrari LaFerrari, Drake pia ameingia Kwenye orodha ya Mastaa Wanaomiliki Ndinga hiyo ambayo vyombo vya Habari vinataja thamani ya gari hiyo kufikia Dola Milioni 7 Za Kimarekani.

Kwenye post yake ya Instagram Aliyotupia Jumapili Drake ameonekana akiwa Na Washikaji Zake Wawili Wakiwa na Ndinga hiyo yenye rangi Ya Njano Na Caption Yake Nikiwa Ni Emoji Ya Limao.