Kendrick Lamar, Drake Na Future Wameikamilisha 40% Ya Usikilizwaji Wa Hip Hop Kwa Mwaka 2017

Katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka, Masikio ya wapenda Muziki yamekaa tayari kusikia ngoma mpya zitakazoanza kuachiwa kutoka kwa wanamuziki wanaowakubali.

Kwa mwaka uliopita Hip Hop imetajwa kama Aina ya Muziki yenye mashabiki wengi kwa Marekani na Duniani kote.

Ingawa 2017 ulikua ni mwaka wenye ngoma nyingi Kali na pia wanamuziki wengi wapya wenye njaa tuliwaona wakifanya poa,

Ripoti ya wanamuziki waliosikilizwa zaidi imetoka na nafasi za juu zimeshikiliwa na wanaHipHop.

Mtandao wa Variety umewataja Future na Drake kama wanamuziki waliosikilizwa Zaidi mwaka 2017.

Ngoma za Drake zimesikilizwa mara Bilioni 6 namba inayomfanya kutajwa kama mwanamuziki pekee kufikisha Idadi hiyo ya wasikilizaji wa mtandaoni ndani ya mwaka mmoja. Future amesikilizwa mara Bilioni 4.2.

Ripoti hiyo imeitaja Humble ya Kendrick Lamar kama ngoma iliyosikilizwa zaidi 2017 ikiwa na wasikilizaji Milioni 555.2.
Hii inaifanya Humble kuwa kinara kati ya nyimbo 16 zilizosikilizwa zaidi ya mara milioni 500 katika kipindi cha mwaka jana.

Takwimu za Variety zinadai Hip Hop imesikilizwa kwa asilimia arobaini (40%) kati ya asilimia zote 100 katika Categories zote za muziki na hakuna category iliyozidi asilimia za Hip Hop.

Hivyo kwa kifupi Hip Hop ndio Muziki ulioongoza Kusikilizwa Zaidi 2017, Mambo yatakuaje 2018?