DRAKE NA FUTURE NDIYO WASANII WALIOSIKILIZWA SANA MWAKA 2017...

Drezzy "Drake" na Future wamechafua ubao.


Kufikia hatua hii kila mmoja amekuwa na shauku ya jinsi namna wasanii watakavyokomeshana 2018, Lakini kwa mwaka 2017, muziki wa Hip Hop umekuwa na nguvu kubwa duniani kwa ujumla hii kutokana na nyimbo ambazo zinatoka na jinsi wasanii wapya wanavyokuja kwa kasi na kufanya kazi kubwa.

Lakini kwa ripoti iliyotoka ni kwamba wasanii waliosikilizwa sana kwa mwka 2017 ni wana Hip Hop, na hao ni Drake na Future. Drake ameshika namba moja huku akiwa amesikilizwa mara billioni 6, kwa mwaka mmoja na kumfanya kuwa msanii wa pekee kuwa na streaming kubwa kwa mwaka mmoja.

Future namba mbili akiwa amesikilizwa mara billioni 4.3 na hiyo ni kutokana na albam tatu alizoachia mwaka 2017. Kendrick lamar akiingiza "HUMBLE'' namba tatu na kufanya kuwa moja ya nyimbo iliyoskilizwa sana mwaka 2017.