Huenda Mr. Davis Ya Gucci Mane Ikafunikwa Na #TheEvilGenius
Gucci Mane ameonekana kuendelea kukifanya kile kinachoitwa kufanya kazi kwa bidii kwa kipindi cha mwaka mmoja ambao amekua uraiani kuanzia mwaka 2016., Kwasasa rapa huyo kutokea Atlanta anafikiri kuuanza mwaka mpya 2018 na wazo la Albamu mpya"The Evil Genius"

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, December 28 Gucci Mane ametupia picha akiwa amepozi nyuma ya "Semi-Truck" huku Caption yake ikisomeka “Next solo album #TheEvilGenius.”
Kwa muonekano huu ni wazi Guwop anaonekana wazi kuwa ameshaikamilisha Albamu hiyo na tunaweza kuhisi hiyo ni moja kati ya Video set zake. 

The Evil Genius inakuja baada ya Mr Davis ambayo ni Albamu ya 11 ya Gucci Mane.