Akaunti Zaidi Ya Bilioni 3 Zilikua Hacked Kwenye Mtandao Wa Yahoo Mwaka 2013


Kampuni inayotoa huduma mbalimbali za kimtandao zikiwemo barua pepe, Yahoo inayomilikiwa na  Verizon ya Marekani imesema akaunti zote Bilioni 3 za watumiaji wake zilikua hacked mwaka 2013,  Baada ya uchunguzi kitendo hicho kilitafsriwa kama tukio kubwa zaidi kuwahi kutokea tofauti na ilivyofikiriwa mwanzo ambapo waliripoti ni akaunti Bilioni 1 tu,

Yahoo imedai kuwa tangazo hili jipya halitishii usalama wa mtandao huo kwani licha yaTaarifa nyingi za wateja wa Yahoo kuibiwa, Taarifa zinazohusiana na masuala ya kibenki zilibaki salama.

Baada ya kuonekana kuandamwa na matatizo ya uvamizi wa kimtandao, Yahoo ilikubali kuiuza kampuni hiyo kwa Dola bilioni 4.8 kwa kampuni ya Verizoni, Lakini baadae kiwango cha pesa kilipunguzwa mpaka kufikia dola bilioni 4.5.JIONGEZE! Utafanyaje ili USIKOSEE Kutuma PESA kwa mtu unayetaka zimfikie na zisiende kwingine?