WIZKID AMEWEKA REKODI YA KUSIKILIZWA ZAIDI KWENYE SPOTIFY 2017 NA KUWAKALISHA MASTAA WA MAREKANI (STREAMS BILLIONI 1.3)


Baada ya kuingia kwenye Guinness Book of Records 2018 na kuweka rekodi hiyo kupitia ngoma ya One Dance iliyokaa namba moja kwenye chati mama za muziki duniani za Billbord Hot 100 kwa shavu la Drizzy Drake, Mkali kutoka Nigeria Wizkid aka Starboy ameoweka rekodi ingine ya kuwa msanii anayeongoza kusikilizwa zaidi kwenye mtandao wa Spotify (The Most-streamed African Artist Ever On Spotify)

Wizkid ameigia kwenye list ya ngoma 100 kali ambazo zimesikilizwa zaidi (mara nyingi zaidi) kwenye mtandao huo wakustream muziki duniani wa Spotify na kusogea mpaka namba 57 kwenye ngoma 100 akiwa na Streams Billioni 1.3 (1, 379, 041, 180) na kuwakalisha wakali wa Marekani kama Pharrel Williams, Big Sean, Pitbull, G Eazy na wengine wa UK.


Utakumbuka mwaka jana Wizkid alingia kwenye list ya wasanii wa itune/Spotify duniani iliyotolewa a Spotify na kupaa kutoka namba 11 hadi namba 3 akiwa mbele ya wakali kama Justin Bieber, Kanye West, Sia, Future, Ty Dollar $ign, The Weekend na wengine kibao huku Drake akiwa namba 1 kwenye list na Rihanna namba 2.

ASLAY 'Sikuwahi KUONGEA Na WCB Kunisaini, Mi Na BEKA FLAVOUR Tunaongea, Hatuwezi kuwa na BEEF'