VIDEO QUEEN WA NATAMBA YA ASALAY, NANA DOLLS AMESEMA AMBER RUTTY NA AGNESS ANGEWAFUNGIA WANACHAFUA FANI

Mrembo aliyeuza 'Nyago' kwenye kichupa cha Msanii Daraja A, Aslay #Natamba ambacho ndio kichupa nambari Moja kwa sasa Tanzania kupitia Mtandao wa YouTube, @nana_dollz amefunguka na kusema kuwa angekuwa na uwezo angewafungia Warembo wenzie Amber Rutty na Agness kwa kuwa wanaidhalilisha tasnia yao kuonekana inaongoza kwa kuwa na Maadili mabaya Mitandaoni.

Akizungumza kupitia kipindi cha Bongo.Home cha Times Fm mapema Jumapili ya wiki iliyopita, @nana_dollz amedai kuwa warembo hao ambao 'wanajinasibu' kung'arisha 'Vibao' kadhaa vya Bongo Flava, hawana maadili ya Kitanzania na ni mfano Mbaya kwa wasichana chipukizi wanaotaka kujiunga na Sana'a ya Ulimbwende katika kiwanda cha Muziki Bongo.

"Sipendi yule Amber Rutty na Mwenzie Agness wanavyojidhalilisha Mitandaoni kwa kweli wanatuharibia na wote tunaonekana wapuuzi kupitia wao, ningekuwa na uwezo ningewafungia wasishiriki kazi yeyote ile" amesema Nana.

Natamba ni video ambayo @nana_dollz amekiri kuwa imemletea mafanikio makubwa ambayo imemfanya kupokea simu kadhaa za mialiko kutoka kwa wasanii wengine.