USICHOKIJUA KUHUSU ALBUM MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ NA NGOMA ZILIZOMO.

Album cover ni kitu kikubwa sana kwenye swala zima la album ya muziki wa msanii, wasanii hutumia muda mrefu zaidi na akili nyingi hadi kukubaliana na  designer wa hizo albums covers kuja kuzikubali. Faida moja wapo ya Album cover kuwa kali na bora inaleta mvuto zaidi wa mnunuzi kuinunua atakapo kutana nayo.

Album cover ya "A Boy From Tandale" inamuonyesha Diamond Platnumz utotoni, akiwa kwenye kitanda, huku ameegemea ukutani, ambako kuna redio yenye kanda ndani, kanda hii ya kianalojia ilikuwa ikitumika kuhifadhia muziki kipindi cha nyuma.


Hii inatuonyesha ni jinsi gani Chibu alianza kuwekwa kwenye mazingira ya muziki tokea kipindi yupo mdogo, hapa heshima apewe mlezi na mzazi wa Chibu Bi. Sandra. Kwenye hii picha kwa makadirio ya kawaida kabisa  Diamond Platnumz alikuwa na umri wa mika kama miwili hivi.


Frame ya Album Cover hii ya Chibu imenakshiwa kwa rangi ya dhahabu, na rangi ya dhahabu inamaanisha mambo mengi sana, kama vile ufalme, utajiri, thamani ya juu, na mwisho ukubwa wa kitu chenyewe.

Jina la Album "A BOY FROM TANDALE" jina ni kali sana, lakini kwanini? Ukilisoma jina na ukiangalia na picha yenyewe inatuonyesha kwamba Chibu anajaribu kutuambia kuwa mvulana mdogo sana aliyekuwa masikini na asiyejulikana kwenye jamii kutokea eneo la Tandale, wilayani Kinondoni kwenye jiji la Dar es Salaam, leo hii ndiyo miongoni mwa vijana wenye power kubwa na ushawishi hapa mjini.

Humu ndani hizi ni baadhi ya ngoma ambazo kwa asilimia kubwa zitakwepo ndani yake. Kutokana na baadhi ya stori nyingi zilizosemekana kama baadhi ya ngoma Chibu angetoka nazo.

1. Halelujah ft Morgan Heritage
2. A Boy From Tandale  ft. Rick Rose ( Aliopost kwenye IG yake)
3. wimbo ft. Maromboso
4. Club banger ft. Wizkid


Kwenye Album Cover limeandikwa neno hili "PARENTAL ADVISORY, EXPLICIT LYRICS"
Hii ina maana gani? ni kwamba, kilichomo ndani kuna mistari ni hatari kwa afya ya mtoto kwa hivyo usimamizi wa mzazi unahitajika.

Hayo ndiyo uliyokuwa huyafahamu kuhusu hii Album mpya ya Chibu, sasa umejua ila kufahamu zaidi kila siku pitia hapa ili ujue jipya ni lipi!.