Unataka Kuishi Ndoto Zako?, Msikilize Diddy Anachokuambia

Licha ya kuwa kimya kwenye muziki kwa muda mrefu lakini bado Ripoti ya Forbes Imemtaja Sean Combs A.K.A Puff Daddy, Puffy, P. Diddy, kama Rappa mwenye mkwanja mrefu unaotajwa kufikia dola milioni 830 za kimarekani sawa na bilioni 186.33 za kitanzania, kutokana na biashara zake ambazo ni, Revolt TV networkMaking the BandP. Diddy's Starmaker na Want to Work for Diddy.

Kupitia ukurasa wake  wa Instagram rapa huyo mwenye umri wa miaka 47 ame-share tips (mbinu) za kile kinachotajwa kuwa imani yake ili kufikia mafanikio.  
 
A post shared by Diddy (@diddy) on


Kama ulivyomsikia Diddy akiongea kwenye video hiyo,Siku zote hakikisha unaamini katika harakati zako,Mawazo chanya ndiyo yatakuwezesha kukuvusha kutoka ulipo mpaka ufikie mafanikio yako na uishi ndoto zako", Mawazo yasiyo na maana kwako yapige chini ufanye unachoona kinakunufaisha. Naamini kama umeelewa hayo machache uliyoyasikia kutoka kwa Diddy unaweza kubadilisha mtazamo wako,pia usisahau kutumia muda wako vizuri.

 TID 'Kutoa nyimbo MARA KWA MARA Ni USHAMBA, Kutokujiamini na Ni UROHO WA Kutaka kusikilizwa':