Toni Kroos 'Nilikuwa sawa kuikacha Man U na kusaini Real Madrid 2014'
TONI KROOS anaamini kuwa alikuwa sawa kuikacha klabu ya soka ya nchini Uingereza Manchester United na kusaini Real Madrid ya nchini Hispania.
Mjerumani huyo alijiunga na Madrid akitokea Bayern Munich kwa dau la Euro Million 20 mwaka 2014.


 "Nimeshinda makombe mawili ya Klabu bingwa ulaya tokea Zidane ajiunge na Timu yetu, tokea mwanzoni amekuwa akinipa ujasiri wa kucheza na kikubwa zaidi amekuwa akinitumia zaidi katika mechi kubwa" Aliongeza Toni ambaye alisajiliwa enzi za kocha Carlo Ancelotti.

Kroos kaja kuwa mmoja kati ya wachezaji wa kuangaliwa sana katika ligi ya La Liga Huku akiwa na magoli nane, akishinda makombe tofauti ikiwemo La Liga, Uefa na Kombe la ligi.

CHEGE Ni kweli umewahi kuwa na mahusiano na VIDEO Queen Tunda?