TIMBULO'SIO KITU KIZURI ALICHOKIFANYA CALISAH'

Mkali wa #SinaHali Timbulo amefunguka na kukemea kwa kile alichokifanya Model Calisah kuvaa viatu vya kike.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Timbulo amepost Video akiwa amevaa Hijab na kuact kama anamtania Calisah itazame hii Video hapa chini uone alichokifanya Mkali Timbulo.


Baada ya kupost hiyo Video nikamvutia waya Mkali Timbulo na kumuuliza je ni kwanini amefanya hivyo na amesema kuwa licha ya kusema Calisah amevuta Mkwanja kwa kupiga picha akiwa amevaa viatu.''mimi kufanya vile ni utani tu,hatuna ushikaji wowote lakini kwa kuwa ni mtu anayefahamika ndiyo maana nimefanya vile,Na unajua likija suala la mkwanja kila mtu anamtazamo wake ambao yeye anao kuna mtu mwingine ukimwambia aue atauwa na mtu mwingine hatofanya hivyo kwa sababu ya hela.Sasa hapo unagundua kuwa watu wengine hawana msimamo wanabadilika kwa sababu ya hela,unajua stail ya hela hiyo ndiyo imewaharibu vijana wengi wa sasa hivi na kufanya vitu visivyo staili kwa ajili ya hela.'' amesema Timbulo

Check picha za Modal Calisah alivyovaa viatu vya kike.

                                                                       Model Calisah
                                                                 Model Calisah