TID MNYAMA ''ALBAM INAUZIKA SOKONI ILA''

Mkali Tid Mnyama anatarajia kuachia Albam yake hivi karibuni lakini amesema kwa upande wake soko la albam kwa Bongo linalipa inategemea na Msanii anavyopromote kazi zake.

Mkali wa 'katika song' Tid Mnyama amesema moja kati ya mipango yake mwaka huu,Atarelease Albam ambayo inaitwa Past Present and Future(PPF).''mimi mwaka huu natarajia kutoa albamu yangu na ni moja kati ya malengo yangu niliyojiwekea mwaka huu,nitaiuza Albamu yangu Online na nitafanya Lounch ya albamu yangu,''Na pia Tid amezungumzia suala ambalo linasemekana kuwa soko la albamu kwa Tanzania bado halifanyi vizuri na amesema kuwa kwamba yeye anadhani kuwa watu hawako serious kwenye kazi zao,''mimi ninachoweza kusema watu hawako serious kwenye kazi zao,unawezaje kutoa nyimbo tatu mfululizo zikafanya vizuri alafu albamu isifanye vizuri,ata hizo nyimbo tatu unaweza ukaziita Mini albamu na ukaiuza sokoni na ukapata pesa.'' Amesema mkali Tid.