Taarifa Za Hali Ya Rappa Young Dolph Baada Ya Kupigwa Risasi Wiki Iliyopita


Young Dolph amejaribu kuwaambia mashabiki zake kama anaendelea vizuri sasa baada ya shambulio la Risasi  lililomjeruhi vibaya wiki iliyopita mitaa ya HollyWood,

Septemba 30, Bigboss huyo wa Route Empire ametumia ukurasa wake wa twitter kuwafahamisha wote waliopokea taarifa hiyo kama maendeleo yake sio mabaya, kwa kutweet Emoji za mnyama Dolphin huku  akimalizia na maneno "Its DOLPH!"

Ripoti za mwanzo zilimtaja Rapa Yo Gotti kama mtuhumiwa  namba moja kwenye tukio hilo lakini baadae ilibainika hakuwemo miongoni mwa wahusika.

Polisi walisema Dolph alikua na ugomvi na kundi la washikaji ambao walikuwepo eneo la tukio, baada ya kujibiShana kwa muda mrefu walianza kutiana vitasa hali ambayo ilipelekea jamaa hao kujawa na hasira na kuamua kumpiga risasi Rapa huyo kutoka pande za Chicago Marekani.

Mbali na ku-tweet kama ishara ya uzima wake, Instagram page yake @YoungDolph imefutwa post zote na ku-Unfollow watu wote, 
CHEGE Ni kweli umewahi kuwa na mahusiano na VIDEO Queen Tunda: