Sikila Ya Madee Na Tekno Imeleta Utata, Dudubaya Kasema Ya Moyoni Madee Nae Kajibu


MSANII wa muziki Bongo Fleva, Madee, anayefanya vizuri na ngoma ‘SEMA’ amemjibu Dudu Baya aliyedai kuwa  ‘Sikila’ si ngoma nzuri.

Kwa mujibu wa GPL, Madee amefunguka juu ya kauli hiyo kuwa anayachukulia maneno hayo ya Dudu Baya kuwa ni maoni yake binafsi kwani hakuna ambaye anafanya kitu bila kupingwa, na msanii hawezi kutoa wimbo ambao kila mtu ataukubali.

“Hatusikii kazi tunasikia maneno tu, kwa hiyo hivyo ni vitu ambavyo kwangu mimi huwa navipisha tu, ukitaka kubishana nakuonyesha kazi yangu hii hapa, nadhani huo ndiyo msingi bora ambao tunatakiwa tuwaelekeze wenzetu wanaojaribu kutoka nje ya mistari,” alisema Madee.

“Wengi ambao nilikua nao, nilianza nao miaka 17 iliyopita ndiyo ambao sasa hatuwasikii, zaidi utawasikia wanaongea hiki na kile, lakini Madee bado anatoa nyimbo na watu wanazipokea vizuri, shoo pia nafanya tena nyingi tu na maisha yanaenda,” amesema Madee

Wimbo wa Sikila ambao Madee kamshirikisha Tekno kutoka nchini Nigeria, video yake ameifanya katika mtindo wa katuni, kitu ambacho Dudu Baya alieleza kuwa hakiendani na Madee aliyemfahamu hapo awali.


Alichokifanya Diamond Platnumz kwenye birthday ya Wema Sepetu, angalia ilivyokua: