NEDY MUSIC:UWEPO WA OMMY DIMPOZ ROCKSTAR 4000 HAKUNIATHIRI


Mkali Nedy Music ambaye ni msanii wa Music label ya Pkp inayomilikiwa na Ommy Dimpoz ameweka wazi kuwa uwepo wa boss wake Rockstar 4000 hakumuathiri.

Ikiwa imetimia miezi mitano tangu Ommy Dimpoz kusaini rasmi kuwa chini ya Music Label ya Rockstar 4000,lakini Ommy Dimpoz pia anamiliki Music label ya Pozi Kwa Pozi(Pkp)ambayo pia anamsimamia Nedy Music,Baada ya maswali ya watu wengi kusema hivi sasa Ommy Dimpoz anaonekana kuwa busy na Rockstar 4000 na kumsahau Nedy Music..,Hatimaye Nedy Music ameongea na kusema kuwa''mimi kwangu haijaniathiri na wala sifikilii kuwa nitaumia kwa uwepo wake RockStar 4000,yeye hakuwa na management ila alinisaini mimi sio vibaya yeye kuwa chini ya Management yeyote ila nadhani ata mimi pia kwangu ni faida kwa sababu ni source ya connection.''ameeleza Nedy Music.

OMMY DIMPOZ AKANA KUJIITA MAJINA YA WANYAMA TAZAMA HAPA AKIHOJIWA NA MTANGAZAJI LILOMMY