MODEL WA BONGO KUONEKANA KWENYE VIDEO MPYA YA DAVIDO


Model wa Bongo Maggie Vampire ametuchana LIVE kuwa ni kweli ataonekana kwenye chupa jipya la mkali kutoka Nigeria, DAVIDO.

Kwenye interview aliyofanya na Lil Ommy kwenye The Playlist Times FM, aliulizwa ile Video Clips aliyoposti kwenye instagram yake yupo na Davido ilikuwa ni Video Shoot wanafanya kwa kuwa yeye ni model na ameshafanya videos na wasanii wa Bongo kama Wakazi, Jux? 

Vampire alisema 'Yeah ni kweli ni video ambayo tumefanya nae, walitaka models kutoka Tanzania kwa kuwa Video tumefanyia Zanzibar, So walitumiwa picha za models 10 kutoka Agency wachague na wakanichangua mimi, baadae tukaenda Zanzibar kufanya shooting, ilikuwa ni experience nzuri sana kwanza, ile kukutana na Davido tu ilikuwa poa sana, kwanza wale wanajali sana. Wanalipa vizuri, Davido ni mtu poa sana. So walisema baada ya week mbili kutoka sasa wanaweza kuiachia, ni wimbo ambao amefanya duet na msanii mungine wa Nigeria ambae ni upcoming. Pia nachati na Mr P (Peter P Square) anajua kuwa ni model so tusikilizie tuone.


ANGALIA INTERVIEW NZIMA ya Maggie Vampire hapa:-