LIZER"HUU NDIO UKWELI JUU YA BEAT YA HALLELUJAH"

Uvumi ambao uko mtaani mpaka sasa juu ya ukweli wa beat ya ngoma ya Diamond-Hallelujah kuwa Producer Lazer sie producer ambae kandaa beat hio taarifa ambazo zipo kitaa ni kwamba Producer Lizer alitumiwa beat akamalizia vitu vichache.

Sasa Lizer mwenyewe kazungumza juu ya hilo na kusema uvumi huo sio wa kweli kwani beat hio ni idea yake kuanzia mwanzo mpaka mwisho na kama kungekuwa na ushirikiano wowote ungejulikana.

"Ile ni beat imetoka kwenye idea ambao nilikuwa nayo na nimeanza kuitengeneza tokea mwanzo mpaka inakamilika hivyo huo uvumi sio wa kweli,"alisema Lizer.
Aidha Lizer alisema uvumi huo unatokana  na watu kutomfatilia kwani kazi kama hizo kaisha fanya sana hivyo WATANZANIA wasubiri mabadiliko makubwa kutoka kwake.

Lizer alisema kwa sasa anategemea kufanya mambo makubwa kutokana na uongozi wa WCB kumwamini kitu ambacho anajivunia.