Lil Wayne Kashitakiwa Kwa Kumkana Mtoto Wake, Huenda Deal Ya Pombe Ikamuokoa


Rappa Lil Wayne huenda akahukumiwa adhabu au faini ya mamilioni iwapo atapatikana na hatia ya kumkana mtoto anaesemekana kuwa ni wa kwake,


Mwanamke mmoja anaefahimika kwa jina la Keiotia Watson amesema aliwahi kum-date rappa huyo lakini mapenzi hayakuendelea baada ya mshikaji kupewa taarifa za ujauzito mwaka 2001.


Keiotia Watson alifungua kesi hiyo miaka 2 iliyopita baada ya kushindwa kumlea mtoto wake kutoka kwa Weezy lakini Mnyamwezi alikana na kutaka apewe vipimo vya DNA, Judge wa nahakama amemuamuru Lil Wayne kuanza kulipa Dola 5 kila mwezi huku akijiandaa kusomewa mashitaka yake,Hata hivyo hiyo inaweza isiwe ishu kubwa kuhusu mtonyo, Kwani Weezy anaonekana kulamba dili kubwa na pombe aina ya "Bumbu"

  
Taarifa rasmi za Wayne kufanya kazi na pombe hiyo hazijawekwa wazi rasmi lakini kwa mujibu wa post yake instagram Lil Wayne ameahsiria kitu kama hicho.

Septemba 27 kwenye Ukurasa wa Instagram wa @OrinalBumbu ilipostiwa picha ya Bosi huyo wa YMCMB akiwa ameshika chupa ya Bumbu na ujumbe wa kumtakia Kheri ya siku ya kuzaliwa.

 

Ikiwa Lil Wayne ameingia kwenye biashara ya Pombe basi atakua ameungana na Marapa wengine kwenye biashara hiyo wakiwemo Drake, Diddy na Rick Ross.