Kendrick Lamar Hashikiki, VMA Alichukua, BET Ametajwa Mara Nyingi, Hii Ya Kusikilizwa Ni Rekodi Nyingine


Kendrick Lamar bado anazidi kuonyesha maajabu kupitia muziki wake, Kwani licha ya kutajwa kama Rappa mwenye Albamu inayosikilizwa zaidi, Ripoti ya nyimbo hamsini zilizosikilizwa zaidi mitandaoni kabla ya mwaka huu kuisha inaonyesha mshikaji anamiliki nyimbo 5 kwenye orodha hiyo.

   Humble ambayo aliitoa kama ngoma ya kwanza kutoka kwenye Albamu "DAMN" ni ngoma namba mbili inayosikilizwa zaidi ikitanguliwa na "Despacito" ya Luis Fonsi, Daddy Yankee, 

Kutoka kwenye "DAMN" nyingine zinazosikilizwa zaidi ni DNA, Love, Element na Loyalty aliyoshirikishwa Badgirl RiRi (Rihanna).   

DAMN Iliingia rasmi sokoni April 11 mwaka huu, ukiangalia vizuri utagundua ni miezi sita tu ya uhai wake lakini inakalisha balaa,

Kutoka Toronto, Canada rapa Drake anaendelea kufanya poa kwenye list hiyo akiwa na jumla ya ngoma 4 zinazosikilizwa zaidi ambazo ni Fake Love, Passion Fruit,Gyalchester na Portland aliyowashikirikisah Travis Scott na Quavo.  

 2017 kwa Kendrick itabaki kuwa kumbukumbu kutokana na makubwa yanayomtokea, Kama utakumbuka mwaka huu mnyamwezi alibeba tuzo tano za VMA kupitia ngoma ya "Humble"  

 Majina ya wanamuziki wa Hip Hop watakaowania Tuzo za BET Hip Hop 2017 yametolewa na Kendrick ameonekana kinara kwa kutajwa mara nyingi akifuatiwa na DJ Khaled pamoja na mrembo Cardi B. 


TID 'Kutoa nyimbo MARA KWA MARA Ni USHAMBA, Kutokujiamini na Ni UROHO WA Kutaka kusikilizwa'