KALAPINA AIBUKA NA KUMPA ZA USO HARMORAPA

Mwanamuziki Kalapina ambaye anasifika sana kwa ubabe kwa wasanii wenzake, kama unakumbuka kitambo kile alipokuwa na bifu na wasanii wengi wenzake wa Bongofleva kipindi hiko akiwa na kundi lake la kikosi cha mizinga ambacho maskani yake yalikuwa Block 41, Kinondoni.


Akiwa kwenye kipindi cha ThePlayList amemponda msanii, mzee wa kiki Harmorapa kuwa ni msanii wa kiki na kimuziki hana lolote, Kala alisema kuwa hajaona chochote kwa msanii kama Harmorapa, kwani hata muziki wake ni mbovu ila Kiki ndizo zilikuwa zinamuweka juu, na mwisho wake ukawa mbaya.


"Kuna yule msanii yule, alikuwa ile siku ya Nape alivyoonyeshwa bastola akakimbia, yule jamaa hamna kitu ni kiki tu ndo zilikuwa zinamuweka juu, hakuna muziki  pale" - Kalapina.