Justin Bieber Mapenzini Na Bebe Mpya?

Ukaribu wa Justin Bieber na kanisa hatimaye umezaa stori nyingine,

Tangu staa huyo wa hitsong "Sorry" alipokatisha ziara zake kimuziki kazi kubwa ambayo imekua ikimchukulia muda kwa sasa ni shughuli mbalimbali za kikanisa ikiwemo mikutano na Ibaada kadhaa.

Muigizaji Paola Paulin ametajwa kwenye tetesi za kutoka kimapenzi na Justin Bieber wanaosemekana kukutana kanisani hapo.

"Wanaonekana Kwenye Mitoko Kadhaa, Wanazunguka Kwenye Gari Pamoja, Watakua Wameanzisha Uhusiano Wa Kimapenzi" Source ya karibu na Bieber Imepenyeza hizo kwa mapaparazi.