Jokate Mwegelo (@JokateM) Uso Kwa Uso Na Kendrick Lamar


Baada ya kutajwa na forbes kama moja ya vijana 30 wenye umri chini ya miaka 30 wajasiriamali kutoka kutoka Africa wanaofanya vizuri, Mwadada Jokate Mwegelo anakutana na Kendrick Lamar, Marekani.

Jokate aliwahi kuposti COVER hiyo na kuandika haya kwenye instagram yake “Looks whose on the cover of Forbes Africa with some other amazing young Africans doing amazing things to create wealth and transform our economies? God is so amazing. 🙏🏽😩❤️🤧.”

Sasa baada ya muda kidogo kupita, Kendrick Lamar ametajwa na forbes kama moja ya wazungumzaji watakaoshiriki kutoa madini zaidi kwa vijana 30 kutoka Africa wenye umri chini ya miaka 30 kwa ajili ya kuwajaza kuwahamasisha zaidi.


Kupitia instagram account ya Jokate, ameposti Video Clip ya kuonesha kuwa tayari wamekutana vijana wote na wapo tayari kupiga stori na watu kibao huku Kendrick Lamar K.Dot akiwa anaangaliwa zaidi kama mtu mwenye ushawishi atakaepiga stori na list ya vijana 30 wajasiriamali kutoka Afrika.


Angalia hapa: