JOKATE AMEFUTA PICHA YA DIAMOND INSTAGRAM


Utakumbuka Baada ya Diamond Platnumz kutoa ngoma yake mpya ya Hallelujah aliyowapa shavu wakali Morgan Heritage, Mwanadada Jokate Mwegelo ambaye aliwahi kudate na Diamond Platnumz aliweka wazi hisia zake za kuikubali ngoma hiyo na kuposti artwork ya ngoma hiyo kwenye page yake ya Instagram ambayo inafollowers Millioni 2 na laki 7 (2.7M) na kushusha ujumbe huu  “Another day. Another $. Another Hit Song Movie from Chibu Dee Baba Dullah @diamondplatnumz @wcb_wasafi ft @morganheritage #Hallelujah.”Sasa Jokate amefuta picha hiyo kwenye Instagram yake ambayo alikuwa kuwatag Diamond, Wasafi na Morgan Heritage.

Katika posti hiyo kabla ya kuifuta, utaona Jokate aliweka utani kidogo kwa Diamond kwa kumwita Baba Dullah - utafahamu mtoto wa Diamond aliyezaa na Mrembo Video Queen na Model Hamisa Mobetto anaitwa Abdulnaseeb (Dullah)

Diamond aliwahi kusema kuwa yuko peace na Jojo wanaongea na kusema kuwa hata VIDEO yake ya i miss you jokate aliaandika subtitles.

Angalia hapa chini:-