Idris Sultan: Sijui Kwanini Tairi Ya Gari Ni Nyeusi, Labda Tumuulize BarakaMshindi wa BBA Hotshots (2014) Mtanzania Idris Sultan amekutana na #NowYouKnow ya Jonijooo ambae ni mtangazaji wa kipindi cha "Chipuka" ya Times FM, Kama ilivyo kawaida ya ya show hiyo ya #NowYouKnow huwa ni maswali yanayoulizwa kutoka kwa mtangazaji kwenda kwa staa anaekuwepo siku hiyo.

 Kwenye show hii Idris Sultan atakuvunja mbavu na majibu aliyotoa kulingana na maswali aliyoulizwa yakiwemo Vitu ambavyo hawezi kutoka bila kuwa navyo, mtu wa mwisho kum-block instagram, matumizi ya pesa, mahusiano yake na vingine kibao.


TID 'Kutoa nyimbo MARA KWA MARA Ni USHAMBA, Kutokujiamini na Ni UROHO WA Kutaka kusikilizwa'