HUU NDIO MSALA AMBAO ALIWAHI KUKUTANA NAO PIGA PICHA WA DIAMOND 'KIFESI'

Ilishakutokea uko sehemu ambayo unataka kupiga picha au kuchukua video alafu camera au simu inazima kwa kuisha charge?Sasa misala kama hio inawatokea sana wapiga picha na muda mwingine anaweza akawa kwenye harusi na tukio linaloendelea ni kukata keki afu camera inakata moto hapo ndio ugumu wa mambo unaanza.

kwa mpiga picha wa Diamond,Kifesi,hali kama hii ilimtokea alipokuwa kwenye Tuzo za MTV South Afrika na lilikuwa ni Tuzo ya mara ya kwanza kwa Diamond ambapo hakupata picha hata moja baada ya camera kuzima ghafla kitu ambacho kumfanya kurudi bongo bila picha hata moja ya tukio hilo.

kifesi anasema tukio hilo ni tukio ambalo hatakuja kulisahau kutokana ilikuwa ni safari yake ya kwanza kwenda South Afrika na Diamond alitoa pesa ya kila kitu ikiwemo ticket na passport lakini anashukuru alivyomchana Diamond juu ya tukio hilo jamaa alichukulia poa na wakayamaliza.