HARMORAPA 'ALIKIBA ANAFANYA MUZIKI BILA KIKI'

Mr kiki Him self Harmorapa amekiri kuwa msanii anaweza kufanya vizuri kwenye Game bila kiki (scandal).

Akihojiwa kwenye kipindi cha Theplaylist cha Timesfm kwa njia ya simu kuhusiana na Topic ya Inbox ambayo imeuliza je msanii anaweza kufanya vizuri bila kiki.Mkali Harmorapa amefunguka na kusema kuwa'inawezekana msanii kufanya vizuri bila kutumia kiki kwa mfano mzuri Alikiba na Fid Q wanafanya vizuri bila kiki,mziki wake unafanya vizuri na anajulikana na wakongwe wengi walikuwa wanafanya vizuri na wengine wapo mpaka sasa wanaimba na hawafanyi kiki hata kidogo,Kiki ni kama kitu cha ziada tu kwa sababu huwezi kufanya kila siku kiki watu watakuchoka.