Hamisa Mobetto amchokoza Zari instagram!

Hamisa, Diamond na Zari picha linaendelea instagram. Hamisa anazifata hereni zake.

Unakumbuka kuna hereni zilionekana madale kwa Diamond ambazo zilidaiwa kuwa ni za Hamisa Mobetto na mama T, Zari the bossylady alimind sana kuzikuta kwenye state house ya Chibu alipodondoka kutoka South Africa.

Sasa Hamisa na Diamond mara nyingi walikuwa wakikanusha kuwa hereni zile sio zake na wala hajui ila leo kupitua instagram yake Hamisa amethibitisha kwa kusema hereni zile ni zake na yupo tayari kuzifata.

Utakumbuka pia Diamond na Zari walifanya Tangazo la Duka la Danube GSM name hereni hizo zilitumika katika tangazo hilo ambalo mama T anamuliza Mondi Kuwa na hereni ni za Danube pia?

Diamond anajikuta na mshangao name tangazo linaisha. Sasa Mobetto aliposti clip ya tangazo hilo na kuandika. "it's about time nifate hereni zangu danube I hope they are still there"

Akimaanisha kuwa ni muda sasa nifate hereni zangu Danube kwa kuwa zilikuwepo wakati wa tangazo, natumai bado zipo.

Hamisa amebidi ajibutue tu instagram kwani nini! Ila hili movie sijui litaishiaje! Kila kukicha kuna drama jipya. Hamisa hivi karibuni katimba mahakamani kumfungulia kesi Diamond kwa madai ya kuzalilishwa na kutopata matunzo ya mtoto.