EX-BOYFRIEND WA KHLOE KARDASHIAN ANA MPENZI MPYA?


Model kutoka Haiti MaddyMorebucks ameonekana mitaa ya Los Angeles siku ya jumatatu October 2 akiwa amemkalia mapajani Ex-Husband wa member wa familia ya The Kardashians, Khloe Kardashian, ambaye alikua ni mchezaji wa mpira wa kikapu nchini marekani Lamar Odom pale walipokuwa wametoka kula chakula cha mchana.

Lakini rafiki wa jirani wa Lamar amesema kuwa Maddy hatoki kimapenzi na Lamar bali ni marafiki tu.Lamar odom ambaye alikumbwa na kashifa ya kutumia madawa ya kulevya ameonekana kudata zaidi baada ya taarifa zinazozidi kusambaa kua ex-wife wake khloe anategemea kupata mtoto na boyfriend wake Tristan Thompson.