Diamond na Rick Ross wanafanya VIDEO ya Collabo yao Marekani

Kwa muda Diamond alitangaza ujio wa Collabo yake na Rapa wa Marekani Rick Ross na sasa Collabo hiyo yanukia na imeiva.

Diamond hivi karibuni alikuwa ameenda Marekani kwenye utoaji wa tuzo za Afrimma na kuibuka Mshindi wa Msanii Bora wa Kiume na kuwaficha Wizkid na Davido kwenye kipengele hicho.

Baada ya zoezi la tuzo kukamilika, kama kawaida yake mtoto wa Tandale Chibu Denga ametumia muda huo kujiongeza na kukutana na Rick Ross On Set kufanya VIDEO ya ngoma yao ambayo aliitangaza muda kuwa itakuja.

Kupitia instagram ya Meneja wake Diamond, Babutale aliposti VIDEO Clip anayoonesha kuwa Diamond anafanya chupa na Rozay Kama behind the scene flani bila sauti, hivyo wimbo hausikiki imekua bad Siri, na Meneja wake Sallam nae aliposti na kusema wapo On Set (Diamond na Rick Ross). Video hiyo inaongozwa na Mr Moe Musa Muongozaji wa Music Videos mkali kutoka Nigeria aliyefanya kazi na Diamond kwenye VIDEO yake ya Hallelujah inayofanya poa kwa sasa kwenye TV Stations na mitandao.

Tusubiri tuone mzigo utadondoka lini, utakumbuka kuwa Rick Ross alimposti Diamond kwenye page yake ya instagram baada ya Chibu kusaini dili kubwa la Belaire na Rosay akiwa moja ya watu wakubwa wanaopush brand hiyo. Rozay aliwahi kupiga ngoma na P Square "Beautiful Onyinye" name kuwa Hit. Hii ya Diamond imewavutia watu wengi na kuisubiri kwa hamu hadi vituo vikubwa vya TV KAMA MTVBase wameposti clip hiyo na kushow kwa Diamond. 

Kumbuka pia Diamond amesaini Universal Music Group.