Bhad Bhabie Kutoka Instagram Mpaka Kuiteka Hip Hop Kama Youngest Female Rapper


Jina lake halisi ni Danielle Bregoli Peskowitz amezaliwa Februari 22, 2003, Hivyo mpaka sasa ana umri wa miaka 14 tu. Umaarufu wake ulianzia mitandaoni alikokua akitupia vipande vya video zenye kampeni yake iliyojulikana kama “Catch Me Outside” baada ya kuonekana kwenye show ya Dr. Phil mwezi Septemba 2016. Ngoma yake ya kwanza "These Hauxe"  aliitambulisha mwezi Agosti mwaka huu na kufanikiwa kushika Namba 77 kwenye chati za Bilboards Hot 100.
Mafanikio ya ngoma hiyo ndiyo yamemfanya dogo huyo kupata Recognition kubwa na kuwashawishi Atlantic Records kumsaini kama rapa mdogo wa kike anaetrend kila kona ya Marekani.
Licha ya kujitahidi kufanya ngoma kali na kuanza kukubalika mapema tabia zake za ubabe na kauli chafu zimeshamfikisha polisi mara kadhaa, Pia aliwahi kunusurika kifungo cha miaka 5 jela.

Unaweza Kuzicheki Ngoma Zake Hapa:


 MADEE kamchana Fid Q na Fid aliuomba wimbo! ROMA akaniambia kwanini umemuimba Fid Q?