BARNABA 'SIUPENDI WIMBO WANGU WA LONELY'

Mkali wa wimbo wa Mapenzi Jeneza na Nampaga Barnaba Classic a.k.a Baba Steve amekiri kuwa haupendi wimbo wake wa lonely.

Baba Steve ameweka wazi kuwa haupendi wimbo wake alioutoa mwaka huu tarehe 24 march 2017 wa Lonely. ''sio kama siupendi wimbo ila kuna vitu vingi vinasababisha nisiupende huu wimbo,na ni wimbo namba moja ninaoupenda kwenye albam yangu. kuna vitu vingi sana vinasababisha niuchukie, ipo video lakini mimi ndiye ninayesababisha video mpaka leo isitoke'' Ameeleza Barnaba.


TAZAMA Hapa BARNABA akihojiwa na Lil Ommy wa Times, Je Ni Kweli AMEPATA MPENZI MPYA?