According To Youtube, Hizi Hapa Ngoma Za Bongo Zinazofanya Poa Zaidi

Kazi kubwa ya lilommy.com ni kukupa info zote za kiburudani zinazoendelea ndani na nje ya Bongo Tanzania, Mastori yote ya mastaa wako unayapata sehemu moja tu. Unachotakiwa kufanya ni kuwa karibu na Social Media ZOTE  kwa jina la lilOmmy.

Wiki iliyopita ngoma kibao za Bongoflava zimeachiwa na the good thing ni kwamba hakuna ngoma ambayo imezingua, Yaani zote zinafanya poa, Kupitia Trending Feed ya mtandao wa youtube tumekusogezea ngoma tano ambazo zimeonekana kuwa na mashabiki wengi zaidi,

5: Harmonize - Nishachoka 

All the way kutoka WCB Wasafi muite Harmonize AKA Raj, Kondeboy, Baba Sarah au Muzee ya wazungu, Ngoma yake "Nishachoka" iliyoachiwa katika mfumo wa Audio ipo kwenye list ya zile video zinazoangaliwa zaidi mtandaoni humo na imepata nafasi ya tano ikiwa na watazamaji zaidi ya 800,000,
4: Rayvanny - Unaibiwa 

Vee Vany Boy, Rayvanny, Baba yake Jaydanny anaendelea kufanya poa na ngoma yake unaibiwa, Tangu kuachiwa kwake Septemba 14 Video yake imeshatazamwa zaidi ya mara 1,500,000

 

3: Ommy Dimpoz - Cheche

Ikiwa ni ngoma yake ya kwanza tangu Kusaini na Rockstar4000, Ommy Dimpoz anaendelea kufanya poa na Cheche ikiwa na watazamaji zaidi ya 400,000

  2:Madee ft Nandy - Sema

 Director Khalmando amehusika kutengeneza Chupa la ngoma "Sema" ya Madee ambayo ndani yake ameonekana Mngarenaro kauvaa uhusika wa Madee akimuimbia African Princess Nandy.

 

1: Diamond Platnumz Ft Morgan Heritage - Hallelujah

 Yeah, ni wazi kama "Hallelujah" ndio ngoma inayofanya poa ndani na nje ya East Africa kwani ukiacha rekodi ambayo ngoma hiyo imejitengenezea ya kutazamwa zaidi ya mara Milioni 1, Diamond Platnumz na Morgan Heritage wameendelea kuishikilia #1 On Trending kwa kipindi chote cha siku 3 ambazo ngoma hiyo imeachiwa kwenye youtube chaneli ya Diamond Platnumz

 

LilOmmyTV pia inakuja na mastori yote ya mastaa, Interviews, na The Playlist ya TimesFM,


CHEGE Ni kweli umewahi kuwa na mahusiano na VIDEO Queen Tunda?