Umewahi Kuwaza Kumsikia Rappa Nicki Minaj Akimsifu Mungu?, Hii Gospel Track Aliyoshirikishwa Na Tasha Cobbs Itakua Kwenye Playlist Yako


Kama ni mfuatiliaji wa Muziki na Waimbaji wa Injili basi jina la "Tasha Cobbs" linaweza kuwa sio geni masikioni mwako,  Kama haumfahamu kwa ufupi anaitwa Natasha Tameika ("Tasha" Cobbs Leonard) muimbaji wa nyimbo za Injili na raia wa Marekani.

Agosti 25 ya mwaka huu Tasha aliiachia Albamu yake "Heart. Passion. Pursuit" yenye jumla ya ngoma 16, ikiwemo "I'm Getting Ready" ambayo rapa Nicki Minaj amefanya kile ambacho tunaweza kukisema ameumiza kwa verse ya kibabe kwa mara ya kwanza kwenye wimbo wa Dini.

Ishu sio Nicki kufanya Gospel, Habari nzuri na njema kwa Tasha na timu yake ni kwamba licha ya kuwa na wiki mbili tu sokoni wimbo huo umetajwa kama wimbo wa Dini uliovunja rekodi ya kufanya Vizuri zaidi kuwahi kutokea kwa mwaka huu.

Mbali na wimbo huo  kuuza kwa muda mfupi Albamu hiyo ya Tasha inaendelea kuzimiliki namba kadhaa kwenye Chati za Billboard kama ifuatavyo:

 #1 Billboard Top Gospel Albums; 
#1 Billboard Top Christian & Gospel Albums;
 #8 Billboard Top Current Albums; 
#10 Billboard Top Digital Albums

Unaweza Kuusikiliza "I'm Getting Ready Ft Nick Minaj Hapa: