Uli-Miss Ladha Ya Craig David?, For The Gram na Heartline Zitakurudishia Vibe Yako.


  Craig Ashley David maarufu Craig David muimbaji, rappa na Producer mwenye asili ya Uingereza, Nyota yake ya muziki iling'aa baada ya kushirikishwa kwenye ngoma Re-Rewind ya Artful Dodger mwaka 1999. Albamu ya kwanza ya Craig David "Born To Do It"  ilikua relesead mwaka 2000.

 

 Craig amewahi kumiliki ngoma 20 kwenye chati za UK Top 40 Singles, Albamu 7 kwenye UK Top 40 Albums kwa mauzo ya zaidi ya copy milioni 15 akiwa kama Solo Artist.

Craig David amekuwa nominated mara 13 kwenye Tuzo za muziki za Uingereza, Mara 4 kama Mwanamuziki Bora Wa Kiume., Grammy Award aliwahi kutajwa kuwania kipengele cha Best Male Pop Vocal Performance.

 Following My Intuition, ni Albamu ya 6 kutoka kwa Craig iliachiwa Septemba 30, 2016 na imeendelea kuwa namba 1 Uk Top 40 Albmus,

Baada ya kuridhika na mapokeo ya Following My Intuition, Craig David ametangaza ujio wa "The Time Is Now"Albamu yake ya 7 Inayotegemewa kuwa sokoni mwaka ujao (2018). Ngoma kama For The Gram na Heartline zimethibitisha uwepo wa Albamu hiyo.


Kwanini Hemedy anajiita Jesus Cousin'?