Young Dee Kuhusu Ngoma Mpya Na Aliyevujisha Picha ZakeHuenda haikuwa wiki nzuri kwa mkali wa hitsong "Bongo Bahati Mbaya" (Young Dee) mara baada ya picha zake za utupu na Video vixen Amber Lulu kusambaa kwa kasi ya 4g kwenye blogs na mitandao ya kijamii mapema siku ya Jumatano. Akipiga stori na gazeti la Mtanzania YoungDaresalama amethibitisha uwepo wa picha hizo na kudai mpaka sasa hajajua aliezivujisha ni nani lakini suala lipo chini ya vyombo vya sheria.

 "Sheria itafuata mkondo wake, Ishu iko polisi tayari wanaendelea na uchunguzi kumbaini aliyezivujisha" 

Young Dee anaetamba na ngoma yake "Bongo Bahati Mbaya" amewaomba radhi mashabiki ambao hawakufurahishwa na picha hizo na kuwaomba wakae tayari kwa wimbo wake mpya.