WATUMIAJI WAFURAHISHWA NA DAWASCO APP:

Watumiaji wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka DAR ES SALAAM (Dawasco) Mkoa wa Tabata wamefurahishwa na mfumo mpya wa 'Dawasco app' umesaidia kurahisisha huduma ya kulipa bill.

  Dawasco app ni mfumo wa mawasiliano unaorahisisha utoaji wa huduma ya maji safi,ambao unamwezesha mteja kupata taarifa za mkwanja wake kila mwezi na huduma ya kuunganishiwa maji.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake katika ofisi za Mkoa Tabata, Aboubakary Tupa amesema kupitia mfumo huo watumiaji watapata taarifa zao kwa wakati.
DAWASCO APP: ni application ya kibabe ambayo itamwezesha mtumiaji kulipia mahitaji yake kwa kupitia simu yake ya mkononi.