Suge Knight anaamini kuwa 2 Pac yupo hai!


Bosi wa Death Row Records Suge Knight, amesema kuwa rapa mkongwe wa muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, 2 Pac Amuru Shakuru huenda yupo hai.

Utakumbuka kuwa siku ambayo 2 Pac anapigwa risasi Sept 7, 1996 alikuwa kwenye gari na Suge Knight na watu wengi walihisi kuwa Suge anahusika na kifo cha Pac kwa kuwa 2 Pac alikuwa anampango wa kuanzisha Makaveli Records baada ya kumaliza mkataba wake na Death Row Records ambayo ni ya Suge Knight, kitu ambacho watu wanahisi kuwa Suge angekosa kupiga mkwanja mwingi zaidi kupitia Pac kama angeondoka Death Row Records na kuanzisha Record label yake.


Lakini mara nyingi sana, rapa 2 Pac amekua akijitabilia kifo chake na kudai kuwa yeye atarudi kama yesu! mfano wimbo wake wa Hearts of Men - 2 Pac anasema 'i died and i came back' nimekufa na nikafufuka, na nyimbo nyingi za Pac amekuwa akisema mara zote kuwa yeye hata akifa atarudi, lakini kuna wimbo wa Thug Mansion - ambao Pac ni kama vile anasound kuwa anaenda kujichimbia sehemu ambayo atapotea na kurudi baadae. Thug Mansion ni sehemu ya maficho ambayo kama vile Pac ataenda kukaa, kujificha ikiwa ndio kama kifo chake na kurudi baadae na kuwa amefufuka.

Sasa kupitia interview aliyoifanya Suge Knight akiwa jela, alivutiwa waya na Mkongwe wa Rap Ice-T na Mkongwe wa Uandishi wa Habari, Soledad O'Brien kupitia Fox kwenye kipengele maalum cha 'Who Shot Biggie & Tupac?' nani kuwauwa Biggie na Pac? na Suge alisema hivi  “When I left that hospital [where Shakur was taken after being shot], me and ‘Pac was laughing and joking,” Tulikuwa tunapiga stori na kucheka na Pac wakati tulivompeleka hospitali baada ya kupigwa risasi.

Alipoulizwa, Je Pac bado yupo hai? alisema kuwa “I’m gonna tell you that with ‘Pac, you never know.” alidai kuwa kwa Pac, huwezi jua!