Stori Ya Mtoto Wa 3 Na Kanye West Haimfurahishi Kabisa Kim Kardashian

Mwanamitindo na Staa wa TV Show ya “Keeping Up With The Kardashians” ambae pia ni mke wa rapa Kanye West hapa namzungumzia Kim Kardashian ameonekana kutokufurahishwa na taarifa zinazosambaa kuhusu yeye na mume wake (Yaani Kanye West) kujipatia mtoto wao wa tatu kwa njia ya upandikizaji.


Akipiga stori na moja ya mtandao maarufu wa mastaa Kim amesema “Nimeona vingi nimesikia mengi sana yakizungumzwa lakini ukweli hatukuwahi kuongea chochote kuhusu ishu hiyo”.


Kwa muda mrefu sasa Kwenye headlines ishu ya mastaa hao  kujipatia mtoto wa kike mwezi Januari mwaka ujao imeendelea kuchukua ukubwa siku hadi siku,


“Nadhani muda maalumu wa kuiongelea ishu hiyo ukifika tutaweka kila kitu wazi, nachukizwa sana na mambo yanayoongelewa midomoni mwa watu wakati sisi kama wahusika hatujathibitisha hilo” Kim aliuambia mtandao huo.


Kwenye miaka 3 ya ndoa yao Kim Kardashian na Kanye West wamejaliwa kuwa na watoto wawili ambao ni North pamoja na Saint West.