Selena Gomez amefanyiwa upasuaji na kuwekewa figo kutoka kwa rafiki yake!

Msanii wa mikato ya Pop marekani na demu wa zamani wa Justin Bieber, Selena Gomez amefanyiwa upasuaji na kuwekewa figo lingine.

Selena ambae ndio msanii namba moja duniani mwenye followers wengi instagram akiwa na idadi ya watu million 127+ Kwa muda amekuwa anasunbuliwa na ugonjwa wa Lupus na ndio maana alishindwa kufanya promotion ya ngoma na kazi zake mpya.

Alibidi Selena afanyiwe upasuaji na kuwekewa figo lingine ili aweze kurudi na kuendelea vizuri na hali yake, alimshukuru sana rafiki yake kipenzi, Francia Raisa aliyejitolea yeye kutolewa figo lake na kukubali awekewe Selena Gomez kitu ambacho kimemfurahisha na kumshangaza sana Selena akawa hana budi kumshukuru kwa kuandika Ujumbe mzito kwenye page yake ya instagram yenye followers million 127.

Pia Gomes alishukru madaktari, familia yake na watu aliokuwa nao katika kipindi kigumu cha ugonjwa na upasuaji wake.

Selena alithibitisha upasuaji huo baada ya kuposti picha akiwa hospitali yeye na rafiki yake (Francia Raisa) aliyetoa figo lake na kumpa rafiki yake. Huu ni Ujumbe wa Selena uliogusa hisia za watu wengi zaidi.

I’m very aware some of my fans had noticed I was laying low for part of the summer and questioning why I wasn’t promoting my new music, which I was extremely proud of.  So I found out I needed to get a kidney transplant due to my Lupus and was recovering. It was what I needed to do for my overall health. I honestly look forward to sharing with you, soon my journey through these past several months as I have always wanted to do with you. Until then I want to publicly thank my family and incredible team of doctors for everything they have done for me prior to and post-surgery.  And finally, there aren’t words to describe how I can possibly thank my beautiful friend Francia Raisa. She gave me the ultimate gift and sacrifice by donating her kidney to me. I am incredibly blessed. I love you so much sis.  Lupus continues to be very misunderstood but progress is being made. For more information regarding Lupus please go to the Lupus Research Alliance website: www.lupusresearch.org/ -by grace through faith