Roma athibitisha Collabo yao na Rapa wa Kenya Khaligraph Jones.

Baada ya kuona picha kwenye mitandao ya jamii zikionesha Roma ameingia studio na rapa mkali kutoka Kenya, Khaligraph, The Playlist ya Times FM ikapiga stori na Roma akiwa nchini Kenya kwenye media tour kujua ni kweli collabo itadonoka soon kutoka kwao au walikutana tu studio kule Kenya kila mmoja akiwa na kazi zake?

Roma "Ni kweli tulienda Kenya kwa muda wa wiki hivi kwa ajili ya kula Eid na kufanya media tour na kukutana na wasanii wa kule kufanya nao collabo na wasanii ambao tumekua tunawasiliana tu,  kwa hiyo tumeshafanya kazi na Khaligraph as ROSTAM na pia Roma kama Roma na wasanii wa huku na Stamina na wasanii wengine pia.... kwa hiyo studio ziko busy sana na pia tulienda na Producer Maneck AM Records ambae nae anashirikiana na producers wa huku. Wasanii weninge tutakao piga nao collano ni Kaka Sungura, Avril na Jaquar pia sema uchaguzi kwa upande wake ulikua unambana"