R.Kelly Totoz Hakuanza Juzi, Back In 1994 Jikumbushe Na Hii...
Mwanamuziki muimbaji R.KELLY amekua akiripotiwa kwenye ishu inayowahusisha wasichana wenye umri mdogo kutoka nae kimapenzi, 
Hivi karibuni kuna wasichana wawili ambao wazazi wao wanaamini watoto wao waliathiriwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki huyo

 Stori hiyo ambayo ilipokelewa kwa mshtuko karibu na kila mtu aliyesikia ilisanua uozo ambao Legendari huyo aliwafanyia wasichana hao waliotajwa kuwa na umri kati ya miaka 18,

 Inasemekana jamaa ali-block kila kitu kuhusu wasichana hao na watu wengine (Ni kama aliwateka hivi) kwani hakuwapa mamlaka ya kuongea wala kuwasiliana na mtu yeyote, 

Kuhusu suala la msosi na mavazi mnyamwezi alikua akihakikisha watoto wanashiba na kupendeza,
Licha ya vyote hivyo kibaya kinachotajwa kuwaharibu zaidi wasichana hao ni Video za ngono alizokua akiwarekodi wakati akifanya nao mapenzi.

Ingawa amekua akitajwa mara nyingi kwenye maskendo kama hayo R.Kelly hajawahi kukamatwa juu ya ishu hizo, Sasa huku na kule mara list ya wasichana wadogo waliotoka na R.Kelly tumeinyaka, Tuanze na hii,

Chapter 1: 1994: R.Kelly Anamuoa Aaliyah Akiwa Na Miaka 15 :

Muimbaji wa zamani Marehemu Aaliyah akiwa na miaka 14 alirekodi Albamu yake ya kwanza “Age Aint Nothing But A Number” hiyo ilikua mwaka 1994, R.Kelly anakadiriwa alikuwa na zaidi ya miaka ishirini, alisimamia kama mwandishi wa Nyimbo. Na hapo ndipo ubuyu wa wawili hao kutoka kimapenzi ukaanza kumwagiaka, Mwaka mmoja baadae Jarida La Vibe lilichapisha Cheti Cha Ndoa ya R.Kelly na Marehemu Aaliyah ambayo ilifungwa kimya kimya na kuuzima uvumi uliotawala kwa muda mrefu.Mwaka 1997 Aaliyah na familia yake walipeleka ombi kuitaka Mahakama ya Michigan ivunje ndoa hiyo baada ya familia ya Aaliyah kutoridhishwa na mienendo ya ndoa hiyo, Kwani Aaliyah alikuwa bado mdogo kuolewa bila ruhusa ya wazazi wake.

 1996 wawili hao walikua wameshavunja rasmi uhusiano wao hali iliyomfanya mnyamwezi R.Kelly Kuisusia “One In A Million” (Albamu ya pili ya Aaliyah), Badala yake akafanya Timbaland,
 
 “Nilishasema, Kwa Heashima Ya Mama Aaliyah ambae ni mgonjwa na Marehemu Baba Yake, Sitaongea chochote kuhusu ndoa yangu na Aaliyah”. Ni moja ya kauli zake kila anpoulizwa maswali kuhusu maisha yake ya ndoa na Aaliyah.

Aaliyah alifariki Agosti 25, 2001 kwenye ajali ya ndege akiwa ni msichana wa miaka 22 tu.

Chapter Yaa 2 Ya Msichana Mdogo aliyetoka na R.KELLY inafuata.

OI, KAMA THE PLAYLIST ILIKUPITA ICHEKI HAPA: