Pharell Williams Kawapigia Magoti Mashabiki Stejini

Mwanamuziki Pharell Williams ameshiriki maandano kulaani mauaji ya mtu mmoja aliyeuliwa mwishoni mwa mwezi Agosti Pande za Charlottesville Marekani.

Akiwa na mizuka mingi baada ya kupiga show ya kibabe, Pharell alipiga magoti stejini huku akisema

"Kama napiga magoti hapa, napiga kwa ajili ya watu wangu, Napiga kwa ajili ya mji wangu, napiga kwa ajili ya bendera ya America inayopepea hapa"

Kitendo cha Pharell kupiga magoti stejini kiliwavutia waandamanaji wengine ambao hawakuonaa shida kumpigia shangwe na kumuunga mkono kwa kupiga magoti kama ishara ya kuomba amani,

Wengine walioungana na Pharell kutoa burudani kwenye maandamano hayo ni wanamuziki J.Cole, Steve Wonder na wachezaji wa timu ya NFL.