P The Mc afunguka kuikubali Seduce Me kuliko ZilipendwaMsanii wa muziki wa hip hop Bongo, P The Mc amefunguka kuipenda zaidi ngoma ya Alikiba ‘Seduce Me’ kuliko Zilipendwa ya Diamond Platnumz/WCB.


Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Mademu Wangu’ ameiambia The Playlist ya Times Fm licha ya kuipenda ngoma hiyo yeye hana upande (team) katika pande hizo mbili.
“Sina team hapo lakini napenda tu atakayefanya kitu kizuri huyo namsapoti. Trending wana miziki miwili, Zilipendwa muziki mzuri, Seduce Me muziki mzuri, lakini nimependa sana Seduce Me, myself!” amesema P The Mc.
“Ni muziki fulani very simple and clear, yaani unaweza kuusikia mara moja na ukaukariri hapo hapo, hauna vitu vingi haukusumbui kuutafuta,” ameongeza.

Seduce Me na Zilipendwa ni ngoma ambazo zimekuwa na ushindani mkubwa tangu zilipotoka August 25 mwaka huu.  Seduce Me hadi sasa katika mtandao wa YouTube ina views milioni 5.6 na Zilipendwa views milioni 5.5.