No More Dramas, The Kardashians Wameamua Kufanya Kweli.....


Producer na Director wa "Keeping Up With The Kardashians" Jeff Jenkins ametumia ukurasa wake wa Twitter kumpongeza Khloe Karadshian kwa kile kinachotajwa kuwa anatarajia kujipatia mtoto wake wa kwanza mwezi Februari mwaka 2018.

Baada ya kuzinguana na Lamar Odon, Kwa takribani mwaka mmoja sasa Khloe amekua akitoka kimapenzi na mchezaji mpira wa kikapu Tristan Thompson na Ofcoz jamaa ametajwa kuhusika.

Well, Taarifa hizo za Khloe kuwa mjamzito zimekuja siku chache baada ya ile ya mdodgo wake wa mwisho "Kylie Jenner" ambae anategemea kupata mtoto wa kwanza na rappa Travis Scott,

Kim Kardashian na Kanye West wanategemea kupata mtoto wa 3 mwezi Januari,2018 kwa njia ya upandikizaji, 

Kourtney Kardashian ambae ni dada mkubwa wa familia hiyo mpaka sasa ana watoto wa kiume watatu huku Rob Kaardashian kaka peke yake kwenye familia hiyo akiwa na mtoto wa kike "Dream" aliyempata kwa mwanamitindo Blac Chyna.

Kendall Jenner anabaki peke yake kama mwanafamilia hiyo asiyekua na mtoto kwa kipindi hiki ambacho kimeonekana kama mastaa hao wa "KUWTK" wameamua kuweka drama pembeni na kuijaza dunia.


Angalia Jinsi P SQUARE Walivyozinguana, Mtiti Mzito!, Kundi Lavunjika: