Njia 3 Ambazo @NikkiWaPili Amezitaja Kama Sababu Ya Wasanii Kujimaliza Wenyewe


Rappa Nikki Wa Pili anaeunda kundi la weusi amekua akitumia Ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter kutoa elimu juu ya mambo mbalimbali ya kwenye jamii hasa yanayowahusu vijana kwa asilimia kubwa.

Leo kupitia elimu zake Nikki ame-share vitu vitatu ambavyo anahisi kama msanii akifanya anakua anaishusha hadhi yake ya usanii,

Kwenye Hii post hapa utaona kulalamikia wasanii wengine, kuwa Jaji wa muziki wa wasanii wengine na kutukana mashabiki ndio vitu rapa huyo amevipa kipaumbele kwenye somo lake.


Well, ukifuatilia vizuri unagundua vitu ambavyo Nikki ametaja vinatokea kwenye maisha ya kila siku, either mitandaoni, kwenye matamasha au hata kwenye Interviews tumekua tukisikia vitu kama hivyo,

Je, kwa mtazamo wako unahisi NikkiWaPili yupo sahihi kwa vitu alivyovitaja, Ni kweli vinawadropisha wasanii?

Kwasasa Nikki anatamba na ngoma yake Kihasara aliyomshirikisha Chin Beez, Kama haujapata fursa ya kuisikia hiki hapa kichupa chake.